Ni vigumu. Mara zote ni vigumu kufanya kitu kwa mara ya kwanza. Hasa kama unashirikiana na wengine, kufanya makosa sio jambo la kushangaza. Tulitaka kurahisisha namna ambavyo wachangiaji wapya wa mifumo ya wazi wanavyojifunza na kuchangia kwa mara ya kwanza.
Kusoma makala na kuangalia mafunzo ya video yaweza kusaidia, lakini ni jambo lipi bora zaidi kuliko kufanya kwa vitendo katika mazingira ya kujifunzia? Mradi huu unalenga kutoa mwongozo na kurahisisha namna ambavyo wachangiaji wapya wanavyoweza kuchangia kwa mara ya kwanza. Ikiwa unataka kuchangia kwa mara ya kwanza , fuata hatua zifuatazo.
Kama haujazoea kutumia 'command line', [waweza kutumia GUI.](#Makala ya namna ya kutumia nyenzo nyingine)
Kama hauna git kwenye kompyuta yako, pakua.
'Fork' repository hii kwa kubonyeza kitufe kilichopo juu ya ukurasa huu Kwa kufanya hivyo nakala ya repository hii itatengenezwa kwenye akaunti yako ya Github.
Sasa clone repository kwenye kompyuta yako. Nenda kwenye akaunti yako ya Github bonyeza kitufe kilichoandikwa clone na baada ya hapo bonyeza kitufe kilichoandikwa copy to clipboard icon.
Fungua terminal >_ kwenye kompyuta yako kisha command ifuatayo:
git clone "url-uliyo-nakili-github"
url hiyo inapatikana kwenye hatua ya ku clone, hakikisha unaondoa fungua semi na funga semi.
Kwa mfano:
git clone https://github.com/jina-lako-unalotumia-Github/first-contributions.git
Kwa kufanya hivyo utakuwa umenakili first-contributions repository kutoka Github kwenda kwenye kompyuta yako.
Kwenye kompyuta yako, ukiwa kwenye terminal ingia kwenye repository uliyonakili
cd first-contributions
Sasa tengeneza branch kwa kutumia command ifuatayo git checkout
command:
git checkout -b <add-your-new-branch-name>
Kwa mfano:
git checkout -b add-luke-oliff
(Jina la branch sio lazima lianze na neno add.)
Sasa fungua faili linaloitwa Contributors.md
, Andika jina lako. Usiweke jina lako mwanzoni au mwishoni mwa faili. Weka sehemu yoyote katikati. Baada ya hapo save faili.
Ukiwa ndani ya directory hii kwenye terminal command ya git status
itakuonesha mabadiliko yote uliyoyafanya.
Jumuisha mabadiliko yote uliyoyafanya kwenye branch uliyotengeneza kwa kutumia command git add
command:
git add Contributors.md
Sasa commit mabadiliko uliyoyafanya kwa kutumia command ya git commit
:
git commit -m "Add <jina> to Contributor list"
Badilisha neno <jina>
na jina lako.
Tuma mabadiliko uliyoyafanya kwa kutumia command ya git push
:
git push origin <jina-la-branch>
Badilisha <jina-la-branch>
na jina la branch ulilotengeneza hapo awali.
Ukiwa Github kwenye repository hii utaona kitufe kilichoandikwa Compare & pull request
. Bonyeza kitufe hicho.
Sasa tuma pull request.
Haitochukua muda mrefu nitaanza kuchukua mabadiliko yaliyofanyika na kuyapeleka kwenye master branch ya mradi huu. Utapokea email kukujulisha mara tu hatua hii itakapokamilika.
Hongera! Umeweza kumaliza hatua za msingi ambazo ni fork -> clone -> edit -> PR ambazo utakutana nazo mara nyingi ukiwa kama mchangiaji!
Sherehekea hatua uliyofikia na wajulishe wengine kwa kwenda kwenye wavuti.
Waweza kujiunga na kundi letu la slack endapo utakuwa unahitaji msaada wowote. Jiunge na kundi letu la slack.
Sasa tuanze kuchangia kwenye miradi mingine. Tumekusanya orodha ya miradi ambayo ina mambo mepesi unayoweza kuanza kushughulika nayo. Angalia Orodha ya miradi.
GitHub Desktop | Visual Studio 2017 | GitKraken | Visual Studio Code | Atlassian Sourcetree | IntelliJ IDEA |